Burkina Faso yatangaza amri ya kutotoka nje usiku kufuatia machafuko
2022-01-24 10:08:00| cri

Burkina Faso yatangaza amri ya kutotoka nje usiku kufuatia machafuko_fororder_VCG111366121500

Burkina Faso imetangaza amri ya kutotoka nje usiku kuanzia saa mbili usiku hadi saa kumi na moja na nusu alfajiri, kufuatia milio ya risasi iliyosikika kwenye kambi kadhaa za jeshi nchini humo mapema jana. Shule kote nchini zinafungwa Jumatatu na Jumanne wiki hii kutokana na agizo lililotolewa na wizara ya elimu.

Serikali ya Burkina Faso imethibitsha kutokea kwa machafuko lakini imekanusha kutokea kwa mapinduzi ya kijeshi. Waziri wa ulinzi wa nchi hiyo Barthelemy Simpore, ametangaza kupitia televisheni ya taifa kwamba hali imedhibitiwa na kukanusha uvumi unaozunguka kwamba rais Roch Marc Christian Kabore ameshikiliwa na jeshi.

 Jumuiya ya Uchumi ya Mataifa ya Afrika Magharibi (ECOWAS) imetoa wito kwa pande zote kutulia na kusisitiza uungaji mkono wake kwa rais Kabore.