Watu 16 wafariki katika moto wa klabu ya usiku mjini Yaounde, Cameroon
2022-01-24 09:13:44| CRI

Ajali ya moto iliyotokea Jumapili saa nane na nusu usiku kwenye klabu moja ya usiku mjini Yaounde, Cameroon, imesababisha vifo vya watu wasiopungua 16.

Waziri wa mawasiliano wa nchi hiyo Rene Emmanuel Sadi,amesema ajali ya moto imesababishwa na milipuko ya fataki zinazotumika katika klabu hiyo. Kwanza moto ulitokea kwenye paa la klabu hiyo, na kusababisha taharuki na kusongamana kwa watu waliokuwa katika klabu hiyo. Watu wanane walijeruhiwa vibaya na kukimbizwa hospitali.

Kwa mujibu wa mashuhuda, watu zaidi ya 100, wengi wao wakiwa ni vijana, walikimbilia lango pekee la kutokea baada ya klabu hiyo kujaa moshi.