Rais wa Zanzibar aunga mkono Michezo ya Olimpiki ya Majira ya baridi ya Beijing ya mwaka 2022
2022-01-24 09:04:18| CRI

Rais wa Tanzania Zanzibar na mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi, amesema kupitia mitandao ya kijamii kuwa anaunga mkono Michezo ya Olimpiki ya Majira ya baridi ya Beijing 2022, na kuitakia mafanikio makubwa michezo hiyo.

Rais Mwinyi amesema anaitakia mafanikio Michezo ya Olimpiki ya Majira ya baridi ya Beijing ya 2022. Amesema Michezo ya Olimpiki ni tamasha kubwa la michezo kwa watu wote duniani, kwa hivyo haipaswi kuingizwa mambo ya siasa, na inapaswa kujiepusha na siasa. Amesema ni kwa kuheshimu moyo wa Olimpiki na kutohusisha mambo ya siasa, ndipo tunaweza kutimiza umoja wa kimataifa na kauli mbiu ya Olimpiki: kasi zaidi, juu zaidi na wenye nguvu zaidi.