Wauaji waua familia ya watu watano katikati ya Tanzania
2022-01-24 09:19:10| CRI

Watu wasiojulikana huko Dodoma, katikati ya Tanzania wamewaua watu watano kutoka familia moja. Kamanda wa polisi kanda ya Dodoma Bw. Onesmo Lyanga amesema waliouawa ni pamoja na mume, mke, watoto wawili na mjukuu.

Bw. Lyanga amewaambia wanahabari kwamba uchunguzi wa mwanzo umeonesha kuwa waliouawa hao walipigwa na kifaa butu. Sasa miili ya wahanga hao imepelekwa katika hospitali kufanyiwa uchunguzi ili kufahamu jinsi walivyouawa.

Ameongeza kuwa baada ya uchunguzi, polisi watatoa taarifa huku akiahidi kuwa polisi watafanya chini juu kuwasaka wauaji hao.