Mlipuko wa mabomu waua watu sita kusini mwa Somalia
2022-01-25 09:28:05| cri

Watu 6 wameuawa na wengine 10 wamejeruhiwa katika mlipuko wa bomu uliotokea Jumatatu wiki hii katika mgahawa mmoja kusini mwa Somalia.

Maofisa wa usalama wamesema mlipuko huo ulitokea Qalimow eneo la Middle Shabelle, kilomita 35 kaskazini mwa mji mkuu Mogadishu.

Hadi sasa hakuna kundi lolote lililodai kuhusika na mashambulizi yaliyotokea hivi karibuni nchini Somalia, lakini wapiganaji wa kundi la al-Shabaab wanafanya mashambulizi kama hayo mjini Mogadishu na sehemu nyingine nchini humo na limeongeza mashambulizi yao japo serikali yake imefanya operesheni kali dhidi ya kundi hilo katikati na kusini mwa nchi hiyo.