Zambia yapokea shehena ya pili ya chanjo ya COVID-19 kutoka China
2022-01-25 09:08:12| CRI

Zambia imepokea dozi laki 4 za chanjo ya COVID-19 iliyotolewa msaada na serikali ya China, ikiwa ni sehemu ya dozi milioni 1 zilizoahidiwa na serikali ya China baada ya makubaliano ya nchi hizo mbili.

Chanjo hiyo ilipokelewa kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kenneth Kaunda na Balozi wa China nchini Zambia Li Jie na waziri wa afya wa Zambia Bibi Sylvia Masebo.

Upande wa China umesema uko tayari kuhamasisha raslimali zaidi ili kuisaidia Zambia kupambana na janga la COVID-19, ikiwa sehemu ya kuonyesha ushirikiano mzuri uliopo kati ya nchi mbili kwa muda mrefu. Msaada wa sasa unafuatia msaada mwingine wa dozi laki 1 zilizotolewa mwaka jana.

Waziri wa afya wa Zambia ameishukuru China kwa msaada huo na kusema umefika kwa wakati, ikiwa nchi hiyo inaanza kutoka dozi ya kuimarisha chanjo, na kutoa chanjo kwa watoto wenye umri wa miaka 12 na zaidi.