Rais wa Malawi avunja baraza la mawaziri
2022-01-25 09:26:25| cri

Rais wa Malawi Lazarus Chakwera amefuta baraza lake la mawaziri Jumatatu wiki hii ambapo kuna habari kuwa wanasiasa wa ngazi wa juu, Idara ya Mahakama na wengine husika wamehusika kwenye kesi moja ya ufisadi inayohusisha mfanyabiashara wa Malawi, Zuneth Sattar, anayeishi Uingereza na sasa inachunguzwa na mamlaka za kupambana na ufisadi za Malawi na Uingereza.

Hatua hiyo inafuatia kuvuja kwa mawasiliano ya simu kati ya mkuu wa Ofisi ya kupambana na ufisadi ya nchi hiyo Bibi Martha Chizuma na mtu asiyejulikana. Rais Lazarus Chakwera ametoa onyo kali kwa Bibi Chizuma kwa kitendo hicho ambacho anakitaja kama ni utovu wa nidhamu.