ECOWAS kufanya mkutano maalumu kutathmini hali ya Burkina Faso
2022-01-26 09:28:38| CRI

Jumuiya ya uchumi ya Nchi za Afrika Magharibi ECOWAS imetoa taarifa ikisema, mkutano maalumu utafanyika katika siku zijazo ili kutathmini hali ya nchini Burkina Faso, kufuatia mapinduzi ya kijeshi nchini humo.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, ECOWAS imesema ingawa jumuiya ya kimataifa na ya kikanda zimetoa wito kwa utulivu na kuheshimu uhalali wa katiba, Burkina Faso imeshuhudia mapinduzi ya kijeshi yaliyofanywa Januari 24, kufuatia kujiuzulu kwa rais Roch Marc Christian Kabore akikabiliwa na tishio, hofu na shinikizo kutoka kwa jeshi baada ya uasi uliodumu kwa siku mbili.

Jumuiya hiyo pia imelaani vikali mapinduzi hayo ya kijeshi, yakiwa alama ya kurudi nyuma kwa demokrasia nchini Burkina Faso.

Wakati huohuo, katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Antonio Guterres amesema, mapinduzi ya kijeshi hayakubaliki katika karne ya 21 wakati akijulisha kwa ufupi kuhusu mapinduzi ya kijeshi yaliyotokea nchini Burkina Faso. Bw. Guterres amesema, jamii za kidemokrasia ni thamani inayotakiwa kulindwa.