Dhoruba ya kitropiki Ana yasababisha vifo viwili katikati ya Msumbiji
2022-01-26 09:34:26| cri

Taasisi ya taifa ya kukabiliana na maafa ya Msumbiji (INGD) imesema dhoruba ya kitropiki iliyopewa jina la Ana iliikumba Msumbiji Jumatatu asubuhi na kusababisha vifo vya watu wawili na wengine 49 kujeruhiwa katika mkoa wa Zambezia, katikati ya nchi hiyo.

Kutokana na mvua kubwa iliyosababishwa na dhoruba hiyo, maji ya mto wa Licungo yalizidi kiwango cha tahadhari cha usalama kwa mita mbili na maeneo ya Namacura na Maganja da Costa yako katika hatari ya mafuriko.

Mamlaka za hali ya hewa zimetabiri kuwa familia zaidi ya 25,000 zitaathiriwa na dhoruba hiyo, na sasa baadhi ya safari za ndege za ndani ya nchi zimesitishwa.