Mapato kutokana na kahawa nchini Kenya kwa mwaka 2021 yaongezeka kutokana na kupanda kwa bei duniani
2022-01-26 09:15:07| CRI

Kupanda kwa bei ya kahawa kwenye soko la dunia mwaka jana, kumeifanya Kenya ipate mapato zaidi kutokana na zao hilo licha ya kupungua kwa kiasi kilichouzwa nje ya nchi.

Mamlaka ya takwimu ya Kenya KNBS imesema Kenya ilipata dola za kimarekani milioni 213 katika kipindi kuanzia Januari hadi Novemba mwaka jana, na kuzidi mapato yote ya mwaka juzi ya dola za kimarekani milioni 196. Licha ya ongezeko hilo la mapato, kiasi cha kahawa iliyouzwa nje kiliendelea kupungua kwa mwaka wa pili mfululizo.

Uzalishaji wa kahawa unapungua kutokana na wakulima wengi wa Kenya kuhamia kwenye mazao mengine hasa maparachichi na Macadamia, huku wengine wakiuza mashamba yao kwa wajenzi wa nyumba.