Kampuni ya China yaanzisha kiwanda cha kuunganisha magari ya betri nchini Rwanda
2022-01-26 09:14:16| CRI

Kampuni ya magari ya Umeme wa China Tailing imeanzisha kiwanda cha kuunganisha pikipiki nchini Rwanda ikiwa ni sehemu ya hatua ya kutoa mchango kwenye juhudi za kupungua utoaji wa hewa ya ukaa na kuhimiza uzalishaji usiosababisha uchafuzi.

Kiwanda hicho katika eneo la viwanda la Gahanga, na limeanza kazi ya uunganishaji, uuzaji na matengenezo ya magari yanayotumia betri. Bidhaa za kampuni hiyo ni pamoja na pikipiki, skuta za betri, na guta za betri.

Mkuu wa kampuni hiyo Bw. Tiger Hoo amesema tofauti na magari yanayotumia mafuta, magari ya betri yanayotengenezwa na kampuni hiyo yanatumia betri kwa asilimia 100. Lengo ni kuwawezesha wanyarwanda kuhamia kwenye mfumo wa usafiri ulio endelevu, safi, wenye ufanisi na wenye gharama nafuu.

Amesema tayari kampuni hiyo imefungua maduka yake nchini Afrika Kusini, Misri, Kenya, Tanzania na Rwanda.