Dhoruba yawaua wavuvi na kusomba mashua 60 za wavuvi visiwani Zanzibar nchini Tanzania
2022-01-26 09:36:45| CRI

Afisa mmoja wa Zanzibar amesema kuwa mvua kubwa na dhoruba visiwani Zanzibar vimeisababisha kifo cha mvuvi mmoja, kuvunja nyumba 190 na kusomba mashua 60 za watalii na wavuvi.

Mkurugenzi wa kamisheni ya kukabiliana na maafa Zanzibar (ZDMC) Bw. Makame Khatib, amesema mvuvi huyo alifariki katika kijiji cha Uroa pwani baada ya kupinduka kwa boti yake kutokana na kupigwa na dhoruba katika Bahari ya Hindi.

Bw. Khatib alisema nyumba nyingi zilizosombwa ziko katika maeneo hatarishi ambayo yamepigwa marufuku kwa ujenzi wa nyumba.