Tanzania yapokea shehena ya pili ya chanjo ya COVID-19 zilizotolewa na China
2022-01-27 09:10:48| CRI

Serikali ya Tanzania imepokea shehena ya pili ya dozi laki za chanjo ya Sinopharm dhidi ya virusi vya Corona iliyotolewa na China.

Chanjo hiyo ilikabidhiwa kwa Waziri wa afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Vijana wa Tanzania Bibi Ummy Mwalimu, na balozi wa China nchini humo Bibi Chen Mingjian kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere mjini Dar es Salaam.

Bibi Mwalimu ameishukuru China kwa mchango huu wa wakati ambao utawasaidia kuharakisha kampeni ya taifa ya kutoa chanjo dhidi ya janga la Corona, na kusema dozi hizo laki nane zitatolewa kwa watu laki nne, na kwamba shehena ya kwanza ya dozi laki tano za chanjo ya Sinopharm ilizotolewa na China Novemba mwaka jana na imetolewa kwa watu laki 2.5.