Mawaziri wa Afrika watahadharisha kuhusu tishio kwa tembo wa misituni
2022-01-27 09:08:09| CRI

Mawaziri wa mazingira wa nchi za Afrika wamesema uwepo wa tembo wa misituni wa Afrika uko hatarini kutokana na ongezeko la matishio yanayotokana na mabadiliko ya tabia nchi, kupungua kwa makazi yao, ujangili na migongano na jamii za wenyeji.

Akiongea kwenye mkutano wa mawaziri wa mazingira kuhusu uhifadhi wa tembo uliofanyika kwa njia ya video, waziri wa Mazingira wa Nigeria Bibi Sharon Ikeazor, amesema uingiliaji madhubuti unatakiwa ili kuwaokoa tembo hao waliobaki, ikiwa ni sehemu ya juhudi za bara zima kuwahifadhi wanyama hao. Amesema kupanua eneo la maeneo yanayohifadhiwa, kuimarisha usimamizi, ushirikishaji wa jamii na utekelezaji wa sheria, ni muhimu katika kuwalinda tembo hao.

Mfuko wa ulinzi wa wanyamapori wenye makao yake mjini Nairobi, pia umesema asilimia 60 ya wanyama hao wameathiriwa na ujangili katika muongo mmoja uliopita.