Jumuiya ya Afrika Mashariki yachukua hatua kupambana na wadudu dhidi ya bidhaa muhimu za kilimo
2022-01-28 09:01:12| CRI

Jumuiya ya Afrika Mashariki imesema imeanzisha programu ya uwezeshaji kwa kujenga vituo vya wakaguzi wa mimea ili kulinda eneo hilo dhidi ya matishio kwa bidhaa muhimu za kilimo.

Taarifa iliyotolewa na makao makuu ya jumuiya mjini Arusha, Tanzania, imesema chini ya mpango huo, wakaguzi wa afya ya mimea watapewa mafunzo kuhusu kazi hiyo, kwenye kufanya uchambuzi wa hatari ya wadudu kwenye mahindi, maharage na mpunga, ambayo ni mazao makuu ya kibiashara katika eneo hilo.

Taarifa hiyo iliyotolewa na Mkurugenzi wa sekta za uzalishaji na za kijamii wa jumuiya hiyo Bw. Jean Baptiste Havugimana, inasema programu hiyo ilizinduliwa kwenye forodha ya Kabanga-Kobero kwenye mpaka kati ya Tanzania na Burundi.