UNICEF yatoa misaada kwa watoto walioathiriwa na dhoruba ya Ana nchini Msumbiji
2022-01-28 09:15:47| cri

Shirika la kuhudumia watoto la Umoja la Mataifa (UNICEF) limetangaza kuwa limeandaa mahali pa kujifunzia kwa ajili ya watoto nchini Msumbiji ambao shule na madarasa yao vimeharibiwa na dhoruba ya Ana.

Shirika hilo limesema kwenye taarifa yake kuwa limepeleka timu ya wataalamu kutoa huduma ya afya na lishe, maji, vifaa vya usafi kwa watoto walioathiriwa na dhoruba hiyo na familia zao.

Takwimu za shirika hilo zimeonyesha kuwa watu karibu 45,000 wakiwemo wanawake na watoto 23,000 wanahitaji msaada wa kibinadamu kufuatia uharibifu uliosababishwa na dhoruba ya Ana katika majimbo mengi nchini humo. Inakadiriwa kuwa dola milioni 3.5 za kimarekani zitahitajika kwa ajili ya misaada kwa watu hao.