AMISOM yaanza mafunzo ya usimamizi wa mali kwa polisi wa Somalia
2022-01-31 17:27:02| cri

Tume ya Umoja wa Afrika nchini Somalia (AMISOM) na washirika wake wamesema wameanza mpango wao wa mafunzo ya wiki mbili ya usimamizi wa kiufundi wa mali kwa maafisa waandamizi na wa ngazi ya kati wa Vikosi vya Polisi vya Somalia (SPF).

Tume hiyo imesema, mafunzo hayo yanayohudhuriwa na maafisa 18 wa SPF kutoka vitengo vya ugavi, mawasiliano, na uchukuzi; na wengine kutoka Kurugenzi ya Mafunzo na Mipango ya SPF, yanalenga kuwasaidia washiriki kuongeza uwezo wao wa kudhibiti kwa ufanisi na kupata ujuzi wa kusimamia mali zote za polisi ya Somalia. 

Kwenye taarifa yake kamanda wa polisi wa AMISOM Augustine Magnus Kailie amesema mali za polisi zinasaidia kuleta ufanisi wa shirika lolote la polisi, na kuongeza kuwa mafunzo hayo yanaruhusu mashirika ya polisi kupata mali, kupokea, kudumisha, kufuatilia na kuhesabu matumizi yao pamoja na kuelewa utaratibu sahihi wa kuteketeza.