CMG yaonyesha Tamasha la Mkesha wa Sikukuu ya Spring barani Afrika
2022-02-02 17:05:21| cri

CMG yaonyesha Tamasha la Mkesha wa Sikukuu ya Spring barani Afrika_fororder_微信图片_20220202154034

Tarehe 31 mwezi Januari, Tamasha lililoandaliwa na Shirika Kuu ya Utangazaji la China (CMG) la Mkesha wa Sikukuu ya Spring na Kukaribisha Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi zilifanyika kwenye jengo la Two Rivers nchini Kenya, ikiwa ni mara ya kwanza kwa Shirika hilo kutangaza moja kwa moja Tamasha la Mkesha wa Sikukuu ya Spring nje ya China kwa mawimbi ya HD 4K.

Magurudumu makubwa ya Ferris barani Afrika yaliwasha taa zenye mwanga mwekundu saa sita kamili usiku kwa saa za Beijing,huku nembo ya CMG na Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Beijing zikioneshwa kwenye Kituo cha Biashara cha Kimataifa.