Rais wa China ahutubia ufunguzi wa mkutano wa 139 wa wajumbe wote wa Kamati ya Olimpiki ya Kimataifa
2022-02-03 16:06:54| cri

Rais wa China ahutubia ufunguzi wa mkutano wa 139 wa wajumbe wote wa Kamati ya Olimpiki ya Kimataifa_fororder_1128325881_16438562514631n

Rais Xi Jinping wa China leo ametoa hotuba kwa njia ya video katika ufunguzi wa mkutano wa 139 wa wajumbe wote wa Kamati ya Olimpiki ya Kimataifa.

Katika hotuba yake, Rais Xi amemkaribisha mwenyekiti wa Kamati hiyo Bw. Thomas Bach pamoja na wajumbe mbalimbali wa kamati hiyo mjini Beijing.

Rais Xi pia ameishukuru Kamati ya Ollimpiki ya Kimataifa kwa mchango wake kwa maendeleo ya michezo nchini China, na uungaji mkono kwa China katika kuomba na kuandaa Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Beijing.