Ofisa wa Umoja wa Afrika asema ushirikiano wa China na Afrika katika sekta za elimu, sayansi na teknolojia uko ndani ya mfumo wa FOCAC
2022-02-03 15:59:19| CRI

Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Elimu katika Idara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Uvumbuzi iliyo chini ya Kamati ya Umoja wa Afrika Bw. Hambani Masheleni amesema, msingi wa ushirikiano na China katika sekta za elimu, sayansi, teknolojia na uvumbuzi unaendana na mfumo wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC).

Masheleni amesema hayo jana jumatano alipoongea na wanahabari mjini Addis Ababa, Ethiopia, kando ya ufunguzi wa Baraza Kuu la Umoja wa Afrika, unaowakutanisha mawaziri wa mambo ya nje wa nchi za Afrika kwa mara ya kwanza tangu kutokea kwa janga la COVID-19.