Kenya yafikiria kuandaa mpango wa mageuzi ya kiuchumi na kijamii
2022-02-03 16:00:58| CRI

Waziri wa Fedha na Mipango nchini Kenya Ukur Yatani amesema nchi hiyo inaandaa mpango utakaosaidia kuongeza kasi ya mageuzi ya kiuchumi na kijamii, na kujenga unyumbufu licha ya athari za janga la COVID-19.

Amesema mpango huo unaoitwa Mpango wa Nne wa Muda wa Kati (MTP) utaanza mwaka 2023 – 2027, na utashirikisha mipango na miradi ya kimkakati inayolenga kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi, usawa wa kijinsia, na matatizo yanayokabili makundi maalum katika jamii.

Pia amesema, serikali ya nchi hiyo itaongeza ushiriki wa sekta binafsi katika utekelezaji wa miradi na mipango hiyo ndani ya mfumo wa ushirikiano wa sekta binafsi na sekta ya umma.