Ofisa wa Umoja wa Afrika aishukuru China kwa msaada wake katika mapambano dhidi ya COVID-19 barani Afrika
2022-02-04 17:25:54| CRI

Ofisa wa Umoja wa Afrika aishukuru China kwa msaada wake katika mapambano dhidi ya COVID-19 barani Afrika_fororder_H.E.-Cessouma-Minata-Samate

Kamishna wa Umoja wa Afrika anayeshughulikia Afya, Masuala ya Kibinadamu na Maendeleo ya Jamii Bibi Samate Minata, amesema China imekuwa ikiusaidia Umoja wa Afrika (AU) na nchi wanachama wake kuondokana na changamoto zilizosababishwa na janga la COVID-19 tangu janga hilo lilipozuka.

Akiongea na wanahabari mjini Addis Ababa Bibi Minata amesema China imekuwa mshirika mzuri wa Afrika katika usimamizi na mapambano dhidi ya janga hili katika bara zima, na ameishukuru kwa msaada ambao imetoa kwa bara zima tangu kulipuka kwa ugonjwa huo.

Amesema bara la Afrika linaagiza takriban asilimia 99 ya chanjo zake za COVID-19 kutoka nje, amesema kwa sasa Umoja wa Afrika na nchi wanachama wake wanafanya kazi ya kuzalisha chanjo barani Afrika, hatua ambayo China imekuwa mshirika mkuu kwenye kazi hiyo.