Watu milioni 13 wakabiliwa na njaa katika pembe ya Afrika
2022-02-09 09:47:48| CRI

Watu milioni 13 wakabiliwa na njaa katika pembe ya Afrika_fororder_非洲之角

Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) limeonya kwamba takriban watu milioni 13 wanakabiliwa na njaa nchini Ethiopia, Kenya, na Somalia, wakati Pembe ya Afrika ikikumbwa na ukame mkubwa unaosababishwa na ukosefu mkubwa wa mvua tangu 1981.

Msemaji wa WFP Tomson Phiri aliwaambia waandishi wa habari Jumanne mjini Geneva kwamba ukame mkubwa umeenea na huenda ukaongezeka zaidi, huku mifugo ikifa, na kusababisha hasara kubwa kwa familia za wafugaji.

Msemaji huyo ameeleza kuwa baada ya mvua kutonyesha kwa misimu mitatu mfululizo, mavuno yalikuwa kwa asilimia 70 chini ya kiwango cha kawaida katika maeneo yaliyoathirika. Aidha alisema bei za vyakula na maji zimepanda na kusababisha kushuka kwa kasi kwa shughuli za biashara.