Zanzibar kupunguza ushuru wa kuagiza sukari kwa silimia 50 ili kukabiliana na mfumuko wa bei
2022-02-09 09:44:57| CRI

Mamlaka ya Tanzania Zanzibar imesema imepunguza ushuru wa kuagiza sukari kutoka nchi za nje kwa silimia 50 ili kukabiliana na mfumuko wa bei na kufanya watumiaji waweze kumudu bidhaa hiyo.

Akitangaza punguzo hilo kwenye mkutano na wanahabari, Waziri wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda wa Zanzibar Omar Said Shaaban, amewaonya wafanya biashara kutotumia vibaya punguzo hilo la ushuru wa kuagiza sukari kwa manufaa yao binafsi. Waziri Shaabani amesema serikali itaendelea kufuatilia bei ya sukari katika soko duniani na kuhakikisha kuwa wafanyabiashara wadanganyifu hawawaadhibu wateja kwa kuwaongezea bei bila sababu yoyote, na pia itawasaka wafanya biashara wote wanaokiuka miongozo ya serikali.