Kenya yafikiria kuanzisha sarafu ya kidijitali ya Benki Kuu
2022-02-11 09:47:24| CRI

Benki ya Apex ya Kenya inaangalia uwezekano wa kuunda sarafu ya kidijitali ya benki kuu (CBDC) ikiitikia matumizi ya kasi ya malipo mbalimbali ya kidijitali nchini.

Kwenye taarifa yake Benki Kuu ya Kenya (CBK) imesema kuna mabadiliko ya malipo duniani, ambayo yanajumuisha pesa za kielektroniki, sarafu zenye thamani tulivu na cryptocurrency nyingine, na hivyo kuongeza mahitaji ya upatikanaji wa sarafu ya kidijitali nchini Kenya. Taarifa imeongeza kuwa njia hizo mpya za malipo zimeibuka ili kurahisisha miamala, na kawaida uwiano wa hatari na faida za sarafu ya kidigitali unatofautiana kutoka uchumi wa nchi moja na nyingine. Katika hatua za kutaka kuanzisha sarafu hiyo, benki ya apex ya Kenya inafuata nyayo za nchi nyingine za Afrika.