IFAD kutoa msaada ili kupunguza athari za COVID-19 nchini Somalia
2022-02-11 09:50:40| CRI

IFAD kutoa msaada ili kupunguza athari za COVID-19 nchini Somalia_fororder_8

Somalia na Mfuko wa Kimataifa wa Maendeleo ya Kilimo (IFAD) wamesaini makubaliano ya msaada wa dola za Kimarekani milioni 1.07 ambayo yatasaidia kukabiliana na ugonjwa wa COVID-19 nchini Somalia.

Pande hizo mbili zilisema katika taarifa ya pamoja iliyotolewa jana mjini Mogadishu kuwa msaada huo utasaidia hatua ya kujikimu kimaisha wa mradi wa COVID-19 RLAC-19, hatua ya kuimarisha uwezo wa watu maskini vijijini kukabiliana na athari za janga hilo na vitisho kwa maisha yao.

Waziri wa kilimo na umwagiliaji wa Somalia Said Hussein Lid alisema nchi kwa sasa inakabiliwa na ongezeko jipya la maambukizi ya COVID-19, huku hali ya ukame ikizidi kuwa mbaya, hivyo msaada wa IFAD kupitia mradi wa RLAC-19 unatolewa ili kupunguza athari katika mazingira magumu.

Hussein alisema sekta ya kilimo imeathiriwa vibaya kutokana na mgogoro na mizozo ya kiuchumi ya miaka mingi, ikichangiwa na COVID-19, ambapo wafugaji wanaojishughulisha na kilimo na wakulima wadogo wameathirika zaidi.