Bunge la Tanzania laitaka serikali kuharakisha kuanzisha huduma za afya kwa wote UHC
2022-02-11 09:48:09| CRI

Bunge la Tanzania limeitaka serikali kuharakisha kuwasilisha mswada unaolenga kuanzisha huduma za afya bora kwa wote (UHC) nchini.

Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii Stanslaus Nyongo, amesema upatikanaji wa UHC utasaidia watu wengi masikini wa nchi hiyo kupata huduma bora za afya. Nyongo amesema maandalizi ya kuwasilisha mswada wa UHC bungeni ambayo yameanza mwaka 2021, yamechukua muda mrefu sana, na kunyima watu haki zao za kupata huduma sahihi za afya. Aidha amesema maandalizi ya mkakati wa taifa wa kufadhili mpango wa UHC yalianza mwaka 2016 lakini baada ya miaka mingi ya majadiliano, serikali bado imechelewa kuwasilisha mswada huo bungeni.