Msomi wa Cameroon: Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Beijing yaakisi mabadiliko makubwa yaliyotokea China
2022-02-14 09:50:48| CRI

Msomi wa Cameroon: Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Beijing yaakisi mabadiliko makubwa yaliyotokea China_fororder_1868644605

Msomi wa Cameroon Dkt. Taling Tene Rodrigue hivi karibuni alipohojiwa na Shirika Kuu la Utangazaji la China CMG, amesema mashindano ya kimataifa ni kiashirio cha uwezo na mustakbali wa maendeleo ya nchi. Kuanzia Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Joto ya Beijing ya mwaka 2008 hadi Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Beijing 2022, mabadiliko makubwa yametokea nchini China katika miaka 14 iliyopita, ambapo China imepiga hatua kubwa katika nyanja za sayansi na teknolojia, utamaduni, uchumi, siasa na michezo.

Dkt. Rodrigue ambaye ni mtafiti mwandamizi wa Taasisi ya Utafiti wa Afrika katika Chuo Kikuu cha Ualimu cha Zhejiang anaona, kwa upande wa dhana, sherehe ya ufunguzi wa Michezo ya Olimpiki ya Mwaka 2008 ilitilia maanani zaidi kufahamisha utamaduni wa jadi wa China, lakini ile ya mwaka huu inazingatia zaidi kufafanua dhana ya Jumuiya ya Binadamu yenye Hatma ya Pamoja. Anaona mabadiliko hayo yanaonesha kuwa China inapenda kushirikiana na dunia ili kutimiza maendeleo na ustawi kwa pamoja, na pia yanaakisi moyo wa wachina kujiamini kwa kina na utamaduni wao na nia yao thabiti ya kushikamana.

Dkt. Rodrigue amesema kwa upande wa teknolojia, matumizi ya teknolojia mbalimbali za hali ya juu, zikiwemo 5G, AR, Cloud Computing na Akili Bandia (AI), ni uvumbuzi mkubwa uliofanyika si kama tu kwenye Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Beijing tu, bali pia kwa mashindano yote ya kimataifa. Anaona, matumizi ya teknolojia hizo ni muhimu na yanatoa usaidizi mkubwa kwenye mazingira maalumu ya sasa ambayo janga la COVID-19 bado linaendelea duniani, na hivyo michezo hiyo kweli inastahili sifa ya “Olimpiki ya Teknolojia za Kisasa”.

Kwa upande wa usalama, Dkt. Rodrigue anaona michezo hiyo inafanyika kwa njia salama licha ya changamoto za maambukizi ya virusi vipya vya Corona. Kufanyika kwa michezo hiyo kumedhihirisha mara nyingine tena mafanikio ya China kwenye mapambano dhidi ya janga hilo. Amesema, Cameroon hivi karibuni iliandaa Makala ya 33 ya kombe la mataifa ya Afrika (AFCON) lililozileta pamoja timu kutoka mataifa 24 ya Afrika na mamia ya maelfu ya mashabiki kutoka sehemu mbalimbali duniani, kwa hivyo anaelewa vizuri ugumu wa kuandaa mashindano makubwa ya kimataifa katika hali ya sasa. Dkt. Rodrigue amesema ndio maana anaipongeza China kwa kuweza kuandaa michezo ya Olimpiki kwa usalama.