Jengo refu zaidi katika Afrika Mashariki lililojengwa na kampuni ya China lakamilika
2022-02-14 09:20:23| cri

Jengo refu zaidi katika Afrika Mashariki lililojengwa na kampuni ya China lakamilika

Jengo refu zaidi katika eneo la Afrika Mashariki yaani jengo la makao makuu mapya ya Benki ya Biashara ya Ethiopia liliojengwa na kampuni ya China CSCEC limekamilika. Jengo hilo liko katikati ya mji wa Addis Ababa likiwa na eneo la mita za mraba elfu 160 na urefu wa mita 209.15.

Waziri mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed na balozi wa China nchini humo Zhao Zhiyuan wamehudhuria sherehe ya kukamilika kwa mradi huo. Akihutubia sherehe hiyo, waziri mkuu Abiy amesema kukamilika kwa jengo hilo kumeonyesha nia ya nchi yake kuhimiza maendeleo ya kisasa katika sekta ya benki.

Mkuu wa Benki ya Biashara ya Ethiopia Bw. Abie Sano anatarajia kuwa jengo hilo litainua ufanisi wa kazi ya benki kwa kiasi kikubwa.

Mtendaji mkuu wa tawi la CSCEC nchini Ethiopia Bw. Zhao Wenjian ameeleza kuwa ujenzi wa mradi huo umetoa ajira zaidi ya 3,000 kwa wenyeji nchini humo.