Israel kuipatia Morocco mfumo wa ulinzi wa anga baada ya makubaliano yenye thamani ya dola milioni 600
2022-02-14 08:41:07| CRI

Kampuni ya mambo ya ulinzi wa anga ya Israel (AIA) itaipatia Morocco mfumo wa kisasa wa ulinzi wa anga na dhidi ya makombora, baada ya kusaini makubaliano yenye thamani ya dola za kimarekani milioni 600.

Kampuni hiyo itaipatia Morocco mfumo wa Barak MX kufuatia makubaliano yaliyofikiwa wakati wa ziara ya waziri wa ulinzi wa Israel Bw. Benny Grantz nchini Morocco mwezi Novemba mwaka jana.

Mfumo wa Barak Mx unaweza kukabiliana na matishio mbalimbali kama vile ndege, makombora ya aina mbalimbali, droni, helikopta na kuweza kukabiliana na shabaha hadi umbali wa kilometa 150.

Morocco na Israel zilisaini makubaliano ya kuanzisha uhusiano wa kidiplomasia mwishoni mwa mwaka 2020, na utekelezaji wa makubaliano haya unakuja wakati Morocco ikiwa kwenye mvutano unaoongezeka na jirani yake Algeria.