Kenya imepokea shehena ya nane na ya mwisho ya msaada wa chakula ulioanza kutolewa mwaka 2008 ili kuimarisha mapambano dhidi ya njaa na utapiamlo ambavyo vimekuwa vikiongezeka kutokana na kutokea kwa ukame wa mara kwa mara.
Waziri wa utumishi wa umma, jinsia, mambo ya wazee na program maalum wa Kenya Bibi Margaret Kobia amesema shehena hiyo una tani 890 za ujazo na itahimiza juhudi kupunguza kukosekana kwa usalama wa chakula katika maeneo yaliyokumbwa na ukame nchini Kenya.
Bibi Kobia amesema Kenya inaishukuru China kwa kuchangia kwenye juhudi za kupunguza njaa nchini Kenya, na tayari msaada huo umesambazwa kwenye maeneo yenye ukame, mbali na kutumiwa kuunga mkono kwenye program za kutoa chakula mashuleni ili kuhimiza lishe kwa watoto.