Msomi wa Sudan Kusini: Dhana ya “Jumuiya ya Binadamu yenye Hatma ya Pamoja” yaendana na mahitaji ya maendeleo ya Afrika
2022-02-15 08:29:29| CRI

Msomi wa Sudan Kusini: Dhana ya “Jumuiya ya Binadamu yenye Hatma ya Pamoja” yaendana na mahitaji ya maendeleo ya Afrika_fororder_1

Mkurugenzi mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Mikakati na Sera ya Sudan Kusini (CSPS) Dkt. Melha Rout Biel amesema, bara la Afrika limebarikiwa kuwa na hazina kubwa ya maliasili, lakini moja ya changamoto kubwa zinazoikabili Afrika ni kukosa dhana ya maendeleo, kwa hiyo dhana ya “Jumuiya ya Binadamu yenye Hatma ya Pamoja” iliyotolewa na China inaendana vizuri na mahitaji ya maendeleo ya Afrika.

Akihojiwa hivi karibuni na Shirika Kuu la Utangazaji la China CMG, Dkt. Biel amesema, dhana ya “Jumuiya ya Binadamu yenye Hatma ya Pamoja” inahitaji uelewa wa kina kutoka kwa viongozi na watu wa nchi zote duniani. Dhana hiyo inaweka uhalisia unaowezekana kutokana na ruwaza kabambe na usimamizi madhubuti wa viongozi wenye maono ya muda mrefu wanaotafuta maguezi ili kuhimiza haki, ushirikishi na ustawi wa pamoja duniani kote.

Dkt. Biel anaona, misaada ya China kwa Afrika si lazima iwe ya kifedha, pia inaweza kuwa ni dhana ya maendeleo yenyewe. Afrika si bara linalokosa maliasili, changamoto yake ni kukosa uongozi wenye mawazo ya kimaendeleo. Amesema kama Afrika itaweza kufuata dhana hiyo ya China, hakika itakuwa mahali bora pa kuishi katika siku zijazo.