Mwenyekiti wa baraza la utawala la Sudan ateua kaimu waziri wa ulinzi
2022-02-15 09:34:26| cri

Mwenyekiti wa baraza la utawala la mpito nchini Sudan Bw. Abdel Fattah Al-Burhan amemteua Jenerali Yassin Ibrahim Yassin, aliyewahi kuwa waziri wa ulinzi wa serikali ya waziri mkuu wa zamani Abdalla Hamdok, kuwa kaimu waziri wa ulinzi.

Bw. Al-Burhan ameteua serikali mpya ya muda inayoundwa na mawaziri 15 tarehe 20 mwezi wa Januari. Sudan imekumbwa na migogoro ya kisiasa baada ya Al-Burhan ambaye pia ni Jenerali wa Jeshi la Sudan kutangaza hali ya dharura mwezi wa Oktoba mwaka jana na kuvunja serikali, hatua iliyosababisha wapinzani kufanya maandamano makubwa mara kwa mara katika mji wa Khartoum na miji mingine nchini humo.