Baraza la Usalama la UM larefusha muda wa jopo la wataalamu kuhusu vikwazo vya Darfur
2022-02-16 08:59:17| CRI

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limeridhia azimio la kurefusha muda wa Jopo la Wataalamu wanaotoa usaidizi kwa Kamati ya Vikwazo vya Darfur hadi kufikia Machi 12, mwaka 2023.

Azimio namba 2620, lililopitishwa kwa kauli moja kwenye baraza hilo lenye wanachama 15, linalitaka jopo hilo kuwasilisha ripoti ya kazi zake kwenye Kamati ya Vikwazo kabla ya Agosti 12 mwaka huu, na kuwasilisha ripoti ya mwisho kuhusu magunduzi na mapendekezo yake kwa Baraza la Usalama kabla ya Januari 13 mwaka kesho.

Azimio hilo pia limelitaka jopo hilo kutoa taarifa kila baada ya miezi mitatu kwenye Kamati ya Vikwazo kuhusu shughuli zake, na kueleza nia ya baraza hilo ya kuchukua hatua zinazofaa kuhusu kurefusha tena muda wa jopo hilo hadi Februari 12, mwaka 2023.