Msomi wa Nigeria: Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Beijing yaonesha China inayojiamini zaidi
2022-02-16 08:33:33| CRI

Msomi wa Nigeria: Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Beijing yaonesha China inayojiamini zaidi_fororder_W020200523719302023896

Msomi wa Nigeria Dkt. Michael Ehizuelen hivi karibuni alipohojiwa na Shirika Kuu la Utangazaji la China CMG, amesema Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Beijing imeonesha China inayojiamini zaidi. Amesema kama tukisema Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Joto ya Beijing ya mwaka 2008 ilionesha China inayoinuka, basi China ya leo haina haja ya kujithibitisha tena.

Dkt. Ehizuelen ambaye ni mtafiti mwandamizi wa Taasisi ya Utafiti wa Afrika katika Chuo Kikuu cha Ualimu cha Zhejiang, amesema kufanyika kwa Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Beijing ni mafanikio mengine makubwa ya watu wa China, ambayo yameufanya Beijing kuwa mji wa kwanza na pekee duniani kuwa mwenyeji wa Michezo ya Olimpiki ya majira ya joto na ya baridi. Amesema, ikilinganishwa na mwaka 2008, Beijing ya leo imeshuhudia mabadiliko makubwa katika pande zote, ambayo urefu wa reli ya chini ya ardhi mjini humo kwa sasa umeongezeka kwa mara tatu, na maendeleo makubwa pia yamepatikana kwenye uhifadhi wa mazingira na ujenzi.

Dkt. Ehizuelen anaona, mabadiliko ya Beijing yanaakisi maendeleo makubwa yaliyoshuhudiwa katika nchi nzima ya China. China ya sasa imekuwa tajiri zaidi na yenye nguvu zaidi kuliko mwaka 2008 ilipoandaa Michezo ya Olimpiki ya majira ya joto, ambapo Pato la Ndani ya Taifa (GDP) limeongezeka kutoka karibu dola trilioni 5 za kimarekani za mwaka 2008 hadi kufikia karibu dola trilioni 18 za mwaka 2021, na China imeinuka kuwa uchumi mkubwa wa pili duniani ikiifuata Marekani. Amesema, China ya leo sio tu ni kiwanda cha dunia, na bali pia imekuwa na makampuni makubwa ya teknolojia za hali ya juu na vituo vya kifedha vya kimataifa, licha ya hayo, China pia inaendeleza mpango wake kakambe wa anga za juu. Mafanikio hayo yote yameifanya China ijiamini na kujivunia na mfumo wake wa siasa, na watu wa China wanajiamini zaidi na mustakbali wa nchi yao kuliko wakati wowote ule, wakiona kuwa ustawi mpya wa taifa la China hauzuiliki.