Kikundi cha madaktari wa China chamsaidia mwanamke wa Sierra Leone kujifungua mapacha
2022-02-16 09:07:20| CRI

Kikundi cha 23 cha madaktari wa China nchini Sierra Leone kimefanikiwa kumsaidia mwanamke mmoja nchini humo kujifungua watoto mapacha wa jinsia tofauti, baada ya kumfanyia upasuaji.

Mkuu wa kikundi hicho Bw. Zhou Xi amesema upasuaji huo ni wa kwanza kufanyika tangu kikundi chake kianze kazi mwaka huu katika hospitali ya urafiki kati ya China na Sierra Leone.

Amesema upasuaji wakati wa kujifungua ni jambo la kawaida katika nchi nyingi lakini ni vigumu kufanyika nchini Sierra Leone kwa sababu kwa kuwa hospitali hiyo imekuwa na uhaba wa damu.

Tangu mwaka huu uanze kikundi hicho kimepokea wagonjwa zaidi ya 500 na kufanya upasuaji mara 30.