China yaisisitiza jumuiya ya kimataifa kuendelea kutoa misaada yenye ujenzi kwa Somalia
2022-02-16 14:56:16| CRI

Naibu mjumbe wa kudumu wa China kwenye Umoja wa Mataifa Bw. Dai Bing jana katika mkutano wa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa alitoa wito akiisisitiza jumuiya ya kimataifa kuendelea kutoa misaada yenye ujenzi kwa Somalia.

Bw. Dai Bing alisema kuwa, siku za karibuni pande zote za Somalia zilitatua matatizo mengi na kuendele kuhimiza mchakato wa uchaguzi. Somalia ilikuwa na mgogoro wa vita katika miaka 30 na bado inakabiliana na changamoto kubwa. Jumuiya ya kimatiafa inapaswa kutoa misaada kwa uchaguzi na ukarabati wa Somalia kwa kushikilia kanuni ya kuongozwa na kumilikiwa na watu wa Somalia, lakini sio kuiwekea vikwazo kwa kupita kiasi.