Tanzania kuimarisha operesheni za zimamoto na uokoaji
2022-02-17 08:29:22| CRI

Serikali ya Tanzania imetenga shilingi bilioni mbili kwa ajili ya manunuzi ya magari ya kisasa ya zimamoto kwa mwaka wa fedha wa 2021/22 ili kuimarisha operesheni za Jeshi la Zimamoto na Uokoaji.

Naibu waziri wa mambo ya ndani Bw. Jumanne Sagini ameliambia bunge mjini Dodoma kuwa idara ya Zimamoto na Uokoaji ya Tanzania inakabiliwa na upungufu wa magari ya zimamoto na vifaa vingine vinavyohitajika kwa ajili ya operesheni zake.

Bw. Sagini amesema serikali imeweka mpango wa kimkakati unaolenga kuimarisha huduma za zimamoto na uokoaji nchini humo, na itaendelea kutenga fedha kila mwaka ili kuhakikisha vifaa vingi zaidi vya kisasa vinapatikana na kusambazwa nchini kote.