Kenya yaweka rekodi kwa kukopa dola milioni 867 za kimarekani kutoka soko la ndani
2022-02-17 08:44:52| CRI

Kenya imekusanya shilingi bilioni 98.6 kutoka soko la ndani kupitia dhamana za taifa ziliyotolewa mwezi huu kuunga mkono bajeti.

Mkurugenzi wa masoko ya kifedha wa Benki ya Apex ya Kenya Bw. David Luusa ametoa taarifa mjini Nairobi, ikisema dhamana zenye thamani ya dola milioni 660 za kimarekani zimerekodi usajili wa asilimia 176, ikiwa alama ya ongezeko la hamasa ya wawekezaji wa ndani na nje. Fedha hizo zilizokusanywa ni juu zaidi kuliko zilizokopwa zamani na serikali kutoka soko la ndani.

Bw. Luusa amesema, benki kuu ilitoa dhamana za serikali Januari 28 na kuvutia zabuni zenye thamani ya dola bilioni 1.16 za kimarekani. Kufuatia kupungua kwa mapato ya kodi na ushuru kulikotokana na maambukizi ya COVID-19, Kenya imeharakisha kukopa pesa kutoka vyanzo vyote vya ndani na nje, ili kufadhili miradi mbalimbali.