Msomi wa Kenya: Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Beijing yaifanya China ipate heshima duniani
2022-02-17 10:22:28| CRI

Msomi wa Kenya: Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Beijing yaifanya China ipate heshima duniani_fororder_2

Shirika la Huduma za Utangazaji la Olimpiki (OBS) limetangaza hivi karibuni kwamba, Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Beijing ni michezo ya majira ya baridi inayotazamwa kwa wingi zaidi katika historia, na imewavutia watu zaidi ya bilioni mbili kwenye mitandao ya kijamii duniani. Msomi na mwandishi wa Kenya Bw. Adhere Cavince alipohojiwa siku za karibuni na Shirika Kuu la Utangazaji la China CMG, amesema, michezo hiyo inavyokaribishwa sana na watazamaji na mashariki wa nchi mbalimbali ikiwemo Marekani, si kama tu inatokana na mvuto mkubwa wa Olimpiki, na bali pia inatokana na uchangamfu maalumu wa michezo hiyo ya Beijing. Anaona mafanikio ya michezo hiyo yameifanya China ipate heshimu duniani.

Bw. Cavince anaona kuwa, mbali na mashindano yenyewe, uchangamfu maalumu wa michezo hiyo ya Beijing kwanza unatokana na matumizi ya teknolojia za hali ya juu, akitolea mfano kuwa viwanja vyote vinatumia nishati safi kwa asilimia 100, magari zaidi ya elfu moja yanayotumia nishati ya hydrogen yanatumika kwenye maeneo yote ya michezo, huku vifaa vingi vya teknolojia za kisasa vikitoa huduma mbalimbali kwa washiriki wa michezo hiyo. Amesema, michezo hiyo ya Beijing pia imetumia teknolojia mpya kupunguza utoaji wa hewa ya ukaa, na kuweka rekodi nyingi ya “mara ya kwanza”katika historia ya Michezo ya Olimpiki.

Bw. Cavince pia anaona, uchangamfu wa michezo ya Olimpiki ya majira ya baridi ya Beijing, pia unatokana na ufuatiliaji mkubwa wa dunia kwa China katika zama za leo. Kuanzia mwaka 2008 Beijing ilipoandaa Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Joto hadi mwaka 2022 inapokuwa tena mwenyeji wa Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi, ushawishi wa China duniani umeinuka kwa kiasi kikubwa kuliko zamani.

Mapema mwaka 2009, China iliipiku Marekani na kuwa mshirika mkubwa zaidi wa biashara kwa Afrika na kudumisha rekodi hiyo hadi leo. Amesema, China ya leo, imetimiza lengo la kupunguza umaskini ambalo ni moja ya Malengo ya Maendeleo Endelevu ya Umoja wa Mataifa, miaka kumi mapema kuliko ilivyopangwa, na pia imejitokeza kuwa mlinzi thabiti wa utaratibu wa pande nyingi, mafungamano ya kiuchumi duniani na mfumo wa kimataifa ambao kiini chake ni Umoja wa Mataifa.

Bw. Cavince amesema, mafanikio ya michezo hiyo inayoendelea Beijing itainua zaidi nguvu ya ushawishi ya China. Ameongeza kuwa, China haikupunguza kasi yake kutokana na janga la COVID-19 na kuandaa michezo hiyo ya Olimpiki kama ilivyopangwa, mafanikio ambayo yamepongezwa na kupewa heshima na nchi mbalimbali duniani. Anaona, Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Beijing imeleta mshikamano wa dunia katika wakati huu wenye changamoto nyingi, na kuweka urithi muhimu wa kutafuta uhodari, umoja na ustawi duniani.