Mwanafunzi wa DRC aonyesha picha aliyochora kwa ajili ya Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Beijing
2022-02-18 09:26:00| cri

Mwanafunzi wa Chuo cha Sanaa cha Jamhuri ya Demokrasia ya Congo (DRC) Bahati Kosi ameonyesha picha aliyochora kwa ajili ya Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Beijing 2022 kwenye Ubalozi wa China nchini humo.

Kosi amesema picha aliyochora inayoonyesha michezo mbalimbali ya majira ya baridi, inaipongeza China kwa kuandaa michezo hiyo kwa mafanikio makubwa licha ya kuwepo kwa changamoto iliyoletwa na janga la COVID-19. Anaona michoro ni moja ya njia ya watu wa nchi yake hasa vijana, kuipongeza China, ambayo imeisaidia nchi yake katika sekta mbalimbali ikiwemo elimu.

Balozi wa China nchini humo Zhu Jing amesema mchoro huo ambao unaonyesha urafiki adimu kati ya DRC na China, na kudhihirisha nia ya pamoja ya kuelekea kwenye mustakabali bora, unakaribishwa sana wakati mwaka huu nchi hizo mbili zinasherehekea miaka 50 tangu mahusiano yao ya kidiplomasia yarudi katika hali ya kawaida.