Kiongozi wa Sudan ataka msukosuko wa kisiasa utatuliwe kwa njia ya mazungumzo
2022-02-18 09:16:17| CRI

Mwenyekiti wa Baraza la Utawala la Mpito nchini Sudan Abdel Fattah Al-Burhan jana Alhamisi alisisitiza nia ya serikali ya kufanya mazungumzo na makundi yote ya kisiasa ili kufikia mwafaka wa pamoja kwa ajili ya kuhakikisha msukosuko uliopo wa kisasa unatatuliwa kwa njia salama.

Bw. Al-Burhan siku hiyo alikutana na mkuu wa Tume ya Umoja wa Mataifa nchini Sudan (UNITAMS) Volker Perthes mjini Khartoum. Kwenye mazungumzo hayo, Bw. Al-Burhan alisisitiza nia na dhamira ya serikali ya kukamilisha mchakato wa mageuzi ya kidemokrasia, na kufanya uchaguzi ulio huru na wa haki na kukabidhi madaraka kwa serikali itakayochaguliwa.