Wachimbaji madini wawili wafariki kwenye mlipuko wa baruti kaskazini mwa Tanzania
2022-02-18 09:18:42| cri

Wachimbaji madini wawili wamefariki dunia katika mlipuko wa baruti mkoani Mara, kaskazini mwa Tanzania.

Diwani wa eneo la ajali Bi. Farida Nchagwa amesema wahanga hao wenye umri wa miaka 20 na 21 walikumbwa na mkasa huo walipochimba dhahabu chini ya ardhi Jumatano wiki hii.

Bi. Nchagwa ametoa wito kwa mamlaka husika kufanya ukaguzi dhidi ya mashimo ya uchimbaji ili kuepusha tukio kama hilo. Amesema mvua kuendelea kunyesha kumeathiri shughuli za uchimbaji wa madini, hasa kwa wale wanaotumia vifaa duni vya uchimbaji.