Sudan Kusini yapongeza maendeleo katika mradi wa televisheni unaosaidiwa na China
2022-02-18 09:17:38| CRI

Ofisa wa Sudan Kusini amepongeza maendeleo makubwa yaliyopatikana na makampuni mawili ya China yanayojenga vituo vya radio na televisheni ya taifa nchini humo.

Mkurugenzi wa Uhandisi katika Shirika la Utangazaji la Sudan Kusini (SSBC) Bw. Ramadan Kamil Abulangi, amesema mradi huo unaotekelezwa kuanzia 2019 utabadilisha huduma za matangazo ya redio na televisheni katika mwezi Agosti.

Bw. Kamil amesema huu ni mradi muhimu zaidi kwa Sudan Kusini na utakuwa wa kwanza au wa pili kwa ukubwa barani Afrika na watu wa Sudan Kusini wataufurahia. Shirika la utangazaji la serikali SSBC litakuwa na chaneli zaidi ya 20, televisheni zote binafsi za Juba zitaunganishwa kwa SSBC.