Msomi wa Nigeria: Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Beijing yatoa jukwaa kwa wanamichezo wa Afrika kutimiza ndoto yao
2022-02-18 09:29:53| CRI

Msomi wa Nigeria: Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Beijing yatoa jukwaa kwa wanamichezo wa Afrika kutimiza ndoto yao_fororder_2129828852

Msomi wa Nigeria Dkt. Michael Ehizuelen hivi karibuni alipohojiwa na Shirika Kuu la Utangazaji la China CMG, amesema ni wanamichezo wachache tu wa Afrika waliowahi kushiriki kwenye michezo ya Olimpiki ya majira ya baridi katika historia, lakini mwaka huu wanamichezo sita kutoka nchi tano za Afrika wameshiriki kwenye Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Beijing, ambayo imetoa jukwaa kwa wanamichezo wa Afrika kutimiza ndoto yao.

Dkt. Michael Ehizuelen ambaye ni mtafiti mwandamizi wa Taasisi ya Utafiti wa Afrika katika Chuo Kikuu cha Ualimu cha Zhejiang, amesema hii ni mara ya kwanza kwa wanamichezo wa Nigeria kushiriki kwenye mashindano ya cross-country skier katika michezo ya Olimpiki ya majira ya baridi, na ni michezo hiyo inayoendelea mjini Beijing ndio imetoa fursa kwa mwanamichezo huyo wa Nigeria kuonesha maendeleo na mustakbali wake. Amesema kwa mwanamichezo binafsi na pia kwa Nigeria, michezo hiyo ya Beijing imewezesha kutimizwa kwa ndoto yao. Anaona michezo hiyo inatoa ujumbe wa mshikamano kwa dunia, na vitendo vya baadhi ya nchi za magharibi kususia kidiplomasia michezo hiyo ya Beijing vinakiuka kidhahiri moyo wa Olimpiki, na kuharibu maslahi ya wanamichezo wa nchi zote ikiwemo Nigeria.

Dkt. Ehizuelen anaona, wakati janga la virusi vya Corona bado linaendelea kote duniani, dunia sasa inahitaji zaidi mshikamano kuliko wakati wowote ule. Michezo ya Olimpiki ya majira ya baridi ya Beijing inayotoa wito wa “kushikamana kwa ajili ya siku zijazo” ni kibwagizo cha mshikamano kwa dunia nzima. Amesema, viongozi zaidi ya 30 wa nchi na mashirika ya kimataifa kuhudhuria ufunguzi wa michezo hiyo, kumedhihirisha kuwa dunia imechoshwa na mgawanyo na makabiliano, bali inahitaji kuimarisha kwa pande zote ushirikiano shirikishi wa kimataifa. China na nchi zilizoshirikI kwenye ufunguzi wa michezo hiyo zimeonesha kivitendo ahadi yao thabiti ya kulinda utaratibu wa pande nyingi na mfumo wa kimataifa ambao Umoja wa Mataifa ni kiini chake, na nia ya pamoja ya kushirikiana kwenye ujenzi wa Jumuiya ya Binadamu yenye Hatma ya Pamoja.