Kenya yasema mimba za faru wawili weupe zimetungwa kutokana na juhudi za kuwaokoa wanyama hao
2022-02-18 09:05:12| CRI

Mamlaka ya Wanyamapori ya Kenya (KWS) imesema mimba mbili za faru weupe zimetungwa kwa ushirikiano na watafiti wa kimataifa kwa lengo la kuwaokoa wanyama hao.

Taarifa iliyotolewa mjini Nairobi na mamlaka hiyo, imesema utungaji huo ulifanyika mwezi Oktoba 2021 na mwezi Februari, na mimba hizo mbili zitahamishiwa kwenye faru mwingine katika siku za karibuni. Taarifa pia inasema hayo ni mafanikio ya saba na ya nane kutokana na ushirikiano wa wanasayansi wa ndani na wa kimataifa.

Juhudi za kuwaokoa faru hao zilianza mwaka 2019 baada ya wanasayansi kuona dalili kuwa na mafanikio.