Watu 3 wafariki katika ajali ya moto katika kambi ya wakimbizi wa ndani kaskazini mashariki mwa Nigeria
2022-02-21 08:27:09| cri

Watu watatu jana wamefariki katika ajali ya moto katika kambi ya wakimbizi wa ndani (IDPs) katika jimbo la Borno, kaskazini mashariki mwa Nigeria.

Mkurugenzi mkuu wa idara ya usimamizi wa dharura katika jimbo hilo, Bw.Yabawa Kolo alisema, moto huo ulisababisha nyumba 3,000 kuharibiwa, huku kaya kadhaa zikikosa makazi.

Amesema moto huo ulioanza katika hema moja, ulienea katika mahema mengine kutokana na kikosi cha zimamoto kuchelewa kufika katika eneo la tukio.