Bwawa kuu la Ethiopia laanza uzalishaji wa umeme
2022-02-21 08:36:54| CRI

Serikali ya Ethiopia imetangaza kuwa bwawa lake kubwa la kuzalisha umeme kwa njia ya maji (GERD) limeanza uzalishaji.

Shirika la Utangazaji nchini Ethiopia (EBC) limesema, Waziri Mkuu wa nchi hiyo Abiy Ahmed alizindua rasmi uzalishaji wa umeme katika bwawa hilo, ambalo linatarajiwa kuwa kituo kikubwa zaidi cha kuzalisha umeme kwa njia ya maji barani Afrika.

Akizungumza katika hafla hiyo, Bw. Abiy amesema uzalishaji wa umeme katika bwawa hilo ni neema kwa nchi nyingine jirani, na kwamba Ethiopia inapanga kusafirisha umeme safi usiochafua mazingira kwenda Ulaya kupitia nchi jirani za Sudan na Misri.

Hatua hiyo inakuja wakati nchi hizo jirani zikiliona Bwawa hilo kama tishio litakalopunguza kiwango cha maji kinachoingia katika nchi zao.