Msomi wa Tanzania: Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Beijing yatoa faraja kwa dunia inayosumbuliwa na janga la Corona
2022-02-22 10:17:06| CRI

Msomi wa Tanzania: Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Beijing yatoa faraja kwa dunia inayosumbuliwa na janga la Corona_fororder_UNIT74_Prof Moshi

Mkurugenzi wa Kituo cha Utafiti wa China katika Chuo kikuu cha Dar es Salaam Prof. Humphrey Moshi amesema, Michezo ya Olimpiki ya Majira Baridi ya Beijing iliyofanyika kwa mafanikio kama ilivyopangwa, ina umuhimu mkubwa wa kihistoria na imetoa faraja kwa dunia inayosumbuliwa na janga la virusi vya Corona.

Akihojiwa hivi karibuni na Shirika Kuu la Utangazaji la China CMG, Prof. Moshi amesema, wakati China ilipopata nafasi ya kuandaa michezo hiyo mwaka 2015, hakukuwa na mtu aliyeweza kujua kwamba michezo hiyo itakabiliwa na changamoto kubwa ambazo hazijawahi kushuhudiwa katika historia. Hivi sasa michezo hiyo imefungwa kwa mafanikio, ushindi ambao unastahili kupewa heshima na watetezi wote wa utandawazi na mfumo wa pande nyingi duniani.

Prof. Moshi amesema mafanikio iliyopata China katika mapambano dhidi ya janga la Corona, yamepunguza kwa kiasi kikubwa viwango vya maambukizi na vifo, na kutia moyo kwa dunia na michezo hiyo. Mbali na hayo, China imetoa msaada wa vifaa tiba na chanjo kwa nchi zaidi ya 150 duniani. Ushiriki wa wanamichezo wapatao 3,000 kutoka nchi na sehemu 91 duniani kwenye michezo hiyo, si kama tu ni pongezi, bali pia ni shukrani kwa juhudi kubwa zilizofanywa na watu wa China kwa ajili ya kuandaa michezo hiyo.

Prof. Moshi anaona, tangu janga la virusi vya Corona lilipolipuka mwaka 2019, dunia nzima imepooza kwenye upande wa usafiri wa watu wa kuvuka mipaka kutokana na hofu, hali ambayo imekwamisha na kupunguza shughuli za sekta mbalimbali, na kuwa na athari nyingi hasi, ikiwemo kudorora kwa uchumi, watu wengi kupoteza ajira na kuongezeka kwa umaskini. Anaona, mafanikio ya Michezo ya Olimpiki ya Majira Baridi ya Beijing yametoa ujumbe wazi kwa dunia kwamba dunia inafufuka polepole na binadamu hakika watalishinda janga la Corona, ujumbe ambao ni faraja kubwa kwa binadamu wote.