Wataalam wa Afrika watoa wito wa uvumbuzi wa kifedha ili kuharakisha mageuzi ya kijani
2022-02-22 08:31:49| cri

 

 

Wataalamu wa Afrika wamesema nchi za bara hilo zinapaswa kupanua matumizi ya fedha za ndani ili kuharakisha mageuzi ya uchumi wa kijani wakati msaada kutoka nchi za nje ukipungua.

Akizungumza kwenye mkutano uliofanyika jana huko Nairobi kwa njia ya video, Mkurugenzi wa teknolojia, mabadiliko ya hali ya hewa na usimamizi wa rasilimali katika Tume ya Uchumi wa Afrika ya Umoja wa Mataifa (UNECA) Bw. Jean-Paul Adam amesisitiza haja ya bara la Afrika ya kuhamasisha rasilimali za ndani katika jitihada za ukuaji wa kijani.

Amesema fedha za hali ya hewa ambazo ni nguzo muhimu ya ukuaji wa Afrika, zinapaswa kulenga rasilimali za ndani ya bara hilo, kwa kuwa  ahadi zinazotolewa na makundi makubwa ya kiuchumi huchukua muda mrefu kutimia.